Matthew 9:18-23

18 aIsa alipokuwa akiwaambia mambo haya, mara akaingia kiongozi wa sinagogi akapiga magoti mbele yake, akamwambia, “Binti yangu amekufa sasa hivi. Lakini njoo uweke mkono wako juu yake, naye atakuwa hai.” 19Isa akaondoka akafuatana naye, nao wanafunzi wake pia wakaandamana naye.

20 bWakati huo huo, mwanamke mmoja, ambaye alikuwa na ugonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, akaja nyuma ya Isa, akagusa upindo wa vazi lake, 21 ckwa maana alisema moyoni mwake, “Kama nikigusa tu vazi lake, nitaponywa.”

22 dIsa akageuka, naye alipomwona akamwambia, “Binti, jipe moyo mkuu, imani yako imekuponya.” Naye yule mwanamke akapona kuanzia saa ile ile.

Isa Amfufua Binti Wa Kiongozi Wa Sinagogi

23 eIsa alipofika nyumbani kwa yule kiongozi wa sinagogi na kuwaona waombolezaji wakipiga filimbi za maombolezo na watu wengi wakipiga kelele,
Copyright information for SwhKC